Psalms 106:8-10

8 aHata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake,
ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu.
9 bAlikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka,
akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.
10 cAliwaokoa mikononi mwa adui;
kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa.
Copyright information for SwhNEN